Nahodha wa
Mbeya City Fc Hassan Mwasapili amesema 2015/16 ndiyo msimu ambao timu
yake itaandika historia mpya ya kushiriki michuano ya kimataifa
inayoandaliwa na shirikisho la soka barani afrika CAF.
Mwasapili ameiambia Tovuti ya
Mbeya City kuwa City imekuwa na mafanikio mazuri kwenye soka la
Tanzania tangu ilipopanda daraja kwa mara ya kwanza 2013/14 na
imefanikiwa kuwa sehemu ya timu nne za juu kwa miaka miwili mfululizo
kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara hivyo ina nafasi kubwa
ya kusogea zaidi hasa ya uzoefu wa miaka hiyo.
“Misimu miwili imetupa uzoefu
wa kutosha, licha ya ugeni tumekuwa kwenye nafasi nne za juu muda wote
tulioingia kwenye ligi, huu ni wakati wa kucheza michuano ya CAF, nia
yetu ni kuweka rekodi nyingine msimu huu mpya, timu yetu bado iko
vizuri licha ya wachache kuondoka, mwalimu amepandisha vijana saba wenye
vipaji vikubwa imani yangu wanakuja kufanya makubwa pengine kuliko
walioondoka ambao nao walikuwa vijana wadogo kama hawa wakati wanaingia
City” alisema Mwasapili
Post a Comment