Ads (728x90)

Tabs

Page


chinese-muslim-brothers
Futari ni mlo ambao waislamu wengi hushirikiana kwa pamoja baada ya siku ndefu ya mfungo kwenye kipindi hiki cha Ramadhan. Kwa watu wengi muda wa Futari huwa mida ya
saa kumi na mbili na nusu jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Lakini kwa wenzetu wa China Futari huliwa muda tofauti na huku kwetu, wenzetu  wa Beijing hufuturu mida ya saa moja na dakika arobaini usiku kwenye Msikiti wa Niujie. Lakini kabla ya kufuturu, watu huandaa vitafunio vichache mbele ya mnara wa msikiti wanapo salia.
chinese-muslim-sisters-preparing-iftar
Vitafunio hivyo ni biskuti, maandazi, tende, kashata, karanga, juice na matikiti maji, na baada ya hapo wanaingia msikitini kusali na baada ya sala hujumuika na watu wengine msikitini hapo kwa ajili ya kupata Futari.
Ripoti ya Pew Foundation kutoka China inasema kwamba, China ina idadi wa waislamu wasiopungua Milioni 23 na wengi wao huishi Kaskazini Magharibi mwa China.

Post a Comment