Riquelme ajutia kutokujiunga na Manchester United
Mchezaji Juan Roman Riquelme wiki hii ameibuka na kutoa ya moyoni pale alipoulizwa na gazeti la michezo la nchini Uhispania, Mundo Deportivo ni kitu gani ana kijutia katika maisha yake ya soka.
Kiungo huyo mshambuliaji wa zamani wa
klabu ya Villarreal ya nchini Hispania na timu ya taifa ya Argentina alikataa ofa ya kujiunga na miamba hiyo ya soka nchini Uingereza, klabu ya Manchester United mwaka 2006.
Kocha wa zamani wa Manchester United, sir Alex Ferguson alijaribu kumshawishi kiungo huyo ‘fundi’ wa mpira kutua Old Trafford lakini Riquelme alikataa na sasa anajuta.
Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona pia anasema, “nilipenda kucheza Villarreal kwa kuwa nilikua huru”. Hata hivyo Riquelme aliamua kurudi nyumbani kwao Argentina 2008 katika klabu ya Boca Junior.
Kushindwa kumtwaa Juan Roman Riquelme, kulimfanya Sir Alex Ferguson amgeukie kiungo Michael Carrick kutoka Tottenham Hotspurs ambaye aimpata mwaka huo 2006 na amekua ni nguzo muhimu katika mafanikio ya klabu hiyo ya mjini Manchester.
Post a Comment