Sentensi nne za Zitto Kabwe akiwataja Watanzania walioficha fedha benki ya Uswis
Jana Zitto Kabwe alikua akiwahutubia wakazi wa jiji la Dar es salaam katika viwanja vya Mwembe Yanga,Temeke na kutaja orodha ya majina ya Watanzania walioficha mabilioni ya fedha katika benki ya Uswis.
Haya ni maneno aliyoyazunguza:-
‘Kuna watu wanasema nyinyi kina zitto na wenzako mnaenda kuanzisha chama uoni utagawa kura za wapinzani sisi ACT tunaenda kutafuta asilimia 58 ya wananchi ambao awapigi kura asilimia 42 tunawaachia wagane wenyewe’…..
‘Kuhusu miswada mitatu ya gesi iliyopelekwa bungeni kwa hati ya dharura ili ipitishwe bungeni, maswala ya mafuta na gesi ni maswala ambayo haitakiwi kufanyiwa haraka ni maswala ambayo yanaitaji concentration kubwa ya wadau wote sio maswala ya kuyapeleka bungeni kwasababu mpo wengi mkayapitisha halafu tukawaingiza watanzania katika matatizo makubwa’.
‘Mwaka 2013 nilienda ufaransa nikakutana na jaji wa ufaransa ambaye alikuwa anafanya uchunguzi kuhusu wafaransa ambao wameficha hela uswizi katika mafaili ambayo alikuwa ameyapata alipata mafaili ya watanzania ambao wameficha hela uswizi akaniita,nikayapeleka serikalini ,benki kuu ya Tanzania, kamishina generali wa TRA na tukampa mwanasherilia mkuu wa serikali tukawaambia hawa ambao hawana uchungu na sisi wanatupa nyaraka hizi kwanini nyinyi amtoi taarifa inavyotakiwa’.
‘Sisi tumepata taarifa kutoka benki moja tawi lake moja benki ya HSBC ya Switzerland ambayo iyo taarifa inawatu 99 watanzania ambao wameweka pesa katika benki hiyo…kwenye taarifa hiyo wengine niwafanyabiashara kiahalali na wengine ni watu ambao wanahusika na kashafa ya pesa za rada ambao walificha pesa katika mabenki ya uswizi’.
Post a Comment