Kwa kipindi cha kama miezi miwili
katikati ya March na May 2015 hali haikuwa nzuri Afrika Kusini,
Xenophobia ilikuwa janga jingine kubwa lililoathiri wageni wengi ndani
ya nchi hiyo.
Kulikuwa na machafuko, mitandaoni
zikasambaa
picha na video zinazoonesha wageni walioko kwenye baadhi ya
maeneo ndani ya nchi hiyo wakivamiwa, walikuwepo waliojeruhiwa.
Wengine waliuawa, wapo waliokimbilia
kuomba hifadhi japo wawe kwenye mikono salama ya Kambi mbalimbali za
Wakimbizi.. lakini wengine waliona South Africa sio mahali salama kwa
ajili yao, walirudi kwenye nchi zao.
Baada ya ripoti zote na hali ya hewa
kukaa sawa, leo nina stori kuhusu watu waliokamatwa wakihusishwa na
kufanya vurugu hizo.. Waziri wa Polisi South Africa, Nathi Nhleko
kaitoa ripoti kwenye Kikao cha Bunge la nchi hiyo kwamba idadi ya watu
waliokamatwa kwa kufanya vurugu na kushiriki kwenye machafuko hayo wako
9,098.
Waziri huyo anasema bado Oparesheni
inaendelea, wanaendelea kuwakamata wahusika wote ila hakutoa ufafanuzi
wowote kuhusu hatua za kisheria zinazochukuliwa kwa watuhumiwa wote.
Post a Comment