Ads (728x90)

Tabs

Page

Adebayor
Mshambuliaji wa kimataifa wa Togo Emmanuel Adebayor, miezi ya hivi karibuni amekuwa na akipitia kipindi kigumu katika klabu yake ya Tottenham Hotspur, huku pia akisakamwa na matatizo ya kifamilia kiasi cha kufikia hatua ya
kuandika katika ukurasa wake wa Facebook .
Mwezi Mei mwaka huu, Tottenham walimpa muda wa mapumziko ili aweze kupata wasaa wa kusuluhisha matatizo yake ya kifamilia.
Huku mustabakali wake na klabu yake ukiwa bado haujulikani, mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal na Manchester City, leo ameamua kusilimu na kuwa Muislamu.
Katika video hapo chini Emmanuel Adebayor, anaonekana akitoa shahada (akishahadia, ishara ya Kiislamu inayoashiria kumkubali Mungu na Muhammad kuwa ndiye Mtume wake), na kuthibitisha kuwa sasa amekuwa Muislamu rasmi.

Post a Comment