Ads (728x90)

Tabs

Page

Kuna njia rahisi za kutengeneza mask ya uso kulingana na ngozi za aina tofauti kwa kutumia asali. Kuna hatua na vitu vinavyohitajika kutengeneza mask ya asali ambapo inatumia muda kidogo. Kwanza unatakiwa kuchagua mask hii ya asali kulingana na ngozi yako.

Kwa ngozi kavu: Mask ya uso ya Parachichi/Ovocado na Asali

Unahitaji:
  • Vijiko 2 vya chakula vya avocado
  • Vijiko 2 vya asali
  • Yai 1 lakini ni kiini/yolk

Ili kuchanganya ingredients hizi pamoja vichanganye vyote kwenye blenda au viponde kwa mikono katika bakuli ili vichanganyike.

Kisha tumia vidole kueneza mask juu ya uso wako mpaka kwenye shingo na iache kwa muda wa dakika 30 kabla ya kuondoa na kisha safisha uso wako kwa maji ya uvuguvugu. Kwa wenye ngozi kavu unatakiwa kufanya mask hii mara moja kwa wiki.

Post a Comment