Mwimbaji kutoka Nijeria ‘Waje’ amesema alijiskia
vibaya sana Psquare walivyopuuzia kumtaja kama msanii aliyeshiriki
kwenye wimbo wao wa ‘Do Me’ uliofanya vizuri Afrika nzima mwaka 2008
kutoka kwenye album yao ya ‘Game Over‘.
Waje hakutajwa kama
msanii aliyeshiriki kwenye wimbo
na hata kwenye video hakuwekwa. Kwenye interview aliyofanyiwa hivi
karibuni Waje amesema “Ukweli ni kwamba
nilijiskia huzuni sana, nilikuwa underground na labda ningetokea kwenye
video ningetoka mapema, ila nasmhukuru Mungu miaka kadha baadae niliweza
kufanya na kutoka mwenyewe“.
Waje aliendelea kusema “P Square hawakunichukua walivyokwenda kufanya video Afrika kusini na hukujua kwanini hakwenda nao“.
Post a Comment