Kitaalam kuna vitu vikitokea
vinasababisha network kuwa na matatizo, basi ikitokea mfano kuna tatizo
kwenye network utasikia mtu analalamika eti Bongo kuna matatizo ya
ajabu, hayo mambo hata Marekani yapo..!!
United Airlines walijikuta wakilazimika
kuzuia safari za ndege kama 75 hivi leo July 08 2015, limetokea tatizo
la network na hali ikawa mbaya kwa kama saa mbili hivi mfululizo, maelfu
ya abiria ilibidi wawe wavumilivu hali ikae sawa.
“Tumepata tatizo la mtandao asubuhi ya leo” >>> huo ndio ujumbe uliotolewa na Msemaji wa Shirika hilo, Luke Punzenberger.
Tatizo lilianza saa mbili asubuhi kwa
saa za New York, likaisha kwenye saa nne hivi… Viwanja vingine abiria
waliingia kabisa kwenye ndege lakini baada ya dharura hiyo ilibidi
washuke, baada ya kila kitu kukaa sawa wakaingia tena na safari
zikaanza.
Post a Comment