Ads (728x90)

Tabs

Page

WALEVI
Wataalamu wa michezo husema ili uwe ‘top athletic’ unahitaji kuwa mbali na pombe pamoja na sigara. Lakini philosophy hii haina mashiko sana hasa kwa kuangalia orodha ya wanamichezo hawa hatari kuwahi kutokea lakini walevi wa kupindukia;

1.Garrincha (1933-1983)
Nyumbani kwao Brazil Garrincha anatajwa kama mmoja wa wanasoka bora zaidi kuwahi kuibariki Brazil kabla ya mchezaji mwenzake Pele. Garrincha ambaye alitwaa kombe la dunia na Brazil 1958 na 1962 alitumia muda mwingi wa maisha yake kunywa sana pombe.
  1. George Best (1946-2005)
Staa huyu kutoka Irend ya kaskazini alikua ni mlevi wa kupindukia. Aliisaidia Manchester United klabu bingwa Ulaya 1968. Alifariki dunia 2005 kwa ugonjwa wa ini.
3.Paul Gascoigne (1967-….)
Moja kati ya wachezaji wenye vipaji zaidi kuwahi kuzaliwa Uingereza. Alitamba sana miaka ya 80′ na mwisho ya miaka ya 90′. Lakini ametumia kila aina ya kilevi ikiwa ni pamoja na kamali. Ameugua mara nyingi kwa sababu za ulevi lakini hadi sasa anaendelea na ulevi.
  1. Ladislao Kubala (1927-2002)
Raia huyu wa Hungari alizaliwa katika kizazi cha dhahabu cha wanasoka adimu duniani lakini alikua akikesha bar kwa ajili ya pombe lakini wakati huo huo alisakata kabumbu la kutisha uwanjani.
  1. Diego Armando Maradona (1960-….)
Huenda ndiye mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea ulimwenguni. Anafahamika ulimwenguni kote kwa kuathirika kwake na madawa ya kulevya. Ni mlevi wa kupindukia lakini hakuna asiyejua ubora wake uwanjani.
  1. Tony Adams (1966-….)
Kwa miaka mingi Adams amekua mlinzi wa kutumainiwa katika klabu yake ya Arsenal na timu ya taifa ya Uingereza. Tony Adams alikuwa ni moja ya wachezaji walioathiriwa na pombe na mara kadhaa amelala bar kwa ulevi.
  1. Socrates (1954-2011)
Mbrazil mwingine huyu aliyependa sana starehe. Alipandikizwa ini kutokana na matatizo ya ugonjwa huo uliotokana na pombe kali. Hata hivyo alikufa kwa matatizo hayo ya pombe kupindukia. Kwa brazil huyu ni moja kati ya wachezaji wa kukumbukwa sana.
8.Jimmy Greaves (1940-…)
Mfungaji bora wa nne wa muda wote wa timu ya taifa ya Uingereza akiwa na magoli 44 kati ya mechi 57. Alikua ni moto wa kuotea mbali mbele ya goli. Alikua mlevi sana kipindi anacheza lakini baadae aliacha na hadi sasa ni mchambuzi wa mpira kwenye televisheni mbalimbali nchini England.
  1. Adriano (1982-….)
Alikua na kila kitu straika wa kisasa anatakiwa kuwa nacho, kasi, nguvu na mbinu(ufundi). Alifanya vizuri mno hususan nchini Italia na hata katika timu ya taifa ya Brazil. Alifunga magoli 31 kati ya mechi 51 za timu ya taifa. Alitabiriwa kufuata nyayo za Romario na De Lima lakini alipenda sana anasa. Mlevi wa kupindukia na hatimaye kurudi kwao kucheza soka na klabu ya Flamengo.
  1. Artem Milevskiy (1985-…)
Raia huyu wa Ukraine alitabiriwa kufuata nyayo za nyota wa zamani wa nchi hiyo na klabu ya AC milan Andrey Shevshenko. Lakini ameshindwa kusajiliwa na klabu kubwa kubwa barani ulaya na sasa anakalia benchi hata katika klabu yake ya kwao ya Dinamo Kiev. Kijana huyu anasifika kwa ulevi wa Vodka na wanawake. Hivi vitu vinatajwa kumharibia uwezo wake wa soka.

Post a Comment