Ads (728x90)

Tabs

Page

..
Ni headline zilizotawala kwenye upande wa muziki wa bendi kuwa mwimbaji na mnenguaji wa muziki wa densi nchini, Hassan Mussa aka Super Nyamwela kuwa amerudi kwenye bendi yake ya zamani maarufu kama Twanga Pepeta.

Sasa leo July 6, 2015 katika mahojiano na millardayo.com alifunguka na kusema ‘Kiukweli kabisa mapokezi yalikuwa ni makubwa sana kwa watu ambao walikuwa wamefika siku ambayo natambulishwa mimi ukumbi ulikuwa umejaa wengi walikuwa hawaamini kuwa mimi na Choki tumerudi Twanga Pepeta lakini nilivyofika pale na kutoa burudani wengi walivyofurahi kiukweli watu na kuna watu ambapo nilikua sijawaona kama takribani ya miaka sita niliwaona siku hiyo’- Super Nyamwela
.
Kwasasa maisha yetu sisi tunaonekana kama vile kwamba wasanii ndio wanakuwa wanaama ama lakini sio sisi tupo kwaajili ya kutengeneza maisha ya familia zetu kwa hiyo ikitokea bendi nyingine siwezi kusema kwamba sitowezi kuhama kwasababu sio nadhili lakini ikitokea bendi ambayo kabisa itanipa maslahi zaidi ya haya na mimi nikaishi na familia yangu vizuri ambavyo ninavyotaka mimi nitakubali kuhama nitaaga  vizuri then mkataba ukiisha nitarudi nyumbani kama kawaida‘- Super Nyamwela
.
.
Mimi nilikuwa katika bendi moja itwayo Extra Bongo ambayo Choki alikuwa kama mkurugenzi na mimi nilikuwa kama kiongozi wa bendi kwa hiyo imedumu mimi niliikutia katikati lakini nimeweza kukaa kwenye bendi takribani ya miaka sita
Mimi nilikuwa naomba niwaambie mashabiki kuwa mimi na choki tumerudi rasmi Twanga Pepeta ninahitaji support tu za watanzania katika kazi zetu pia cha kumalizia naomba watanzania wawe na uzalendo wa kuelewa nyimbo za wasanii wa ndani kisha zifuate za nje’- Super Nyamwela

Post a Comment