Ni utamaduni wa kawaida kabisa na
uliozoeleka ikitokea kuna harusi hivi basi kadi za michango zinapitishwa
na watu wanatoa chochote ili kusaidia kufanikisha tukio hilo.
Nimefikiwa na hii ya China
, unajua kitu kinaitwa Beijing Size Olympic Wedding Expo? umewahi kusikia chochote kuhusu hilo?
Beijing Size Olympic Wedding Expo ni mnada unaofanyika mara tatu kila mwaka ndani ya China…
hapo kinaletwa kila kitu kinachohusiana na harusi, iwe ni magauni,
suti, pete, mapambo, hadi magari ya maharusi unaweza kuvipata kwenye
mnada huo.
Wenyewe wanasema lengo hasa la kufanya
mnada huo ni kusaidia kupunguza gharama za matumizi ya pesa zinazotumika
kuaanda sherehe hizo.
Lakini kuna baadhi ya Wachina wanaona
kuwa mnada huu bado ni kitu cha bei kubwa kwao,wao wameamua kuanzisha
style mpya ya kufunga ndoa zinazoitwa Do-It-Yourself Wedding! Aina hizi za harusi hufanyika majumbani na ndugu, jamaa na marafiki.
Harusi za namna hii hazihitaji mialiko
kwani mialiko hutolewa kwa njia ya tangazo la bango kwenda kwa ndugu
jamaa na marafiki, na MC anaweza kuwa mtu yoyote aliyealikwa. Chakula
kinapikwa na wanafamilia na suala la vinywaji linasimamiwa na marafiki.
Nimekusogezea baadhi ya picha za mnada huo pamoja na baadhi ya picha za aina hii ya Do-It-Yourself Wedding.
Post a Comment