Pep Guardiola ni Kocha ambaye anaifundisha Klabu ya Bayern Munich, kwani ana mpango wa kuifundisha Timu yoyote ya Taifa? Dani Alves kafungua haya mengine yaliyokuwa kwenye moyo wa Kocha huyo.
Beki wa pembeni wa klabu ya FC Barcelona ya Hispania Dani Alves amethibitisha dhamira ya kocha wake wa zamani wa klabu hiyo Pep Guardiola kutaka kuinoa timu ya taifa ya Brazil.
Alves
alilaumu kwa kusema maafisa wa soka wa shirikisho la soka Brazil CBF
waliogopa kumuajiri Kocha wa kigeni katika nafasi ya timu ya taifa.
“Pep alisema
anataka kuipa Brazil ubingwa wa dunia na alikuwa na mbinu thabiti za
kutufanya sisi kushinda kombe la dunia… Maafisa wa shirikisho hilo
hawakutaka sababu hawakujua kama Wabrazil wangekubali timu yao ya taifa
ifundishwe na kocha wa kigeni” >>> Dani Alves.
Hata hivyo FC Barcelona chini ya Pep Guardiola imeshinda mataji 14 ikiwemo mawili ya klabu bingwa barani ulaya ndani ya misimu minne.
Pep Guardiola aliondoka FC Barcelona mwaka 2012 na alichaguliwa kuwa kocha wa Bayern Munich ya Ujerumani katika kipindi cha usajili cha majira ya joto na kutwaa mataji kadhaa akiwa anaifundisha klabu hiyo.
Hata hivyo jumatano hii Brazil itakuwa
inakumbuka siku ya kipigo cha karne cha kufungwa mabao 7-1 na timu ya
taifa ya Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia
lililofanyika mwaka jana nchini Brazil.
Post a Comment