Wakati hekaheka za usajili
zikiwa zimepamba moto barani Ulaya, wababe wa soka nchini Uturuki
Galatasaray, wamethibitisha kumsajili mshambuliaji wa zamani wa
Arsenal, Bayern Munich na Inter Milan Lukas Podolski kwa ada ya pauni
milioni mbili na nusu.
milioni mbili na nusu.
Podolski ,30, ambaye alijiunga
na Arsenal miaka mitatu iliyopita amekuwa na wakati mgumu klabuni hapo
mara baada ya kukosa nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza, hali
iliyopelekea kutolewa kwa mkopo kwenda Inter Milan ya nchini Italia.
“Tulikuwa na mazungumzo mazuri na Wenger,” Touihri aliliambia gazeti la Bild la nchini Ujerumani.
“Bado alitaka kumbakisha Lukas
klabuni lakini alishindwa kumhakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza.
Ndio maana tukafikia muafaka katika zoezi hili.”
Podolski amefunga mara mbili dhidi ya Galatasaray katika mchuano ya vilabu bingwa Ulaya msimu uliopita
Post a Comment