Kundi maarufu la muziki kutoka Nigeria P Square
wanazidi kuvuna mafanikio yao mengi wanayoyapata kupitia muziki… hivi
karibuni kundi hilo lilipata fursa ya kutembelea ofisi za rapper Jay Z nchini Marekani, New York na kufanya nae interview pamoja na mkutano!
P Square walikuwa nchini Marekani kwa ajili ya tour na baada ya kurudi nyumbani Peter Okoye mmoja ya wasanii wanaounda kundi la P Square alichukuwa time na kupost kwenye account yake ya Instagram miongoni mwa mafanikio walioyapata kwenye tour ya safari hii huko Marekani kwa kupost picha na ujumbe uliosema…
>>> “Kwenye ofisi za @tidal na ilikuwa interview na mkutano poa sana. #SomethingBig #RocNations”.<<< @peterpsquare.
Miezi michache iliyopita Jay Z alimtuma binamu yake Bee High huko Nigeria
kwenda kutafuta soko na wasanii ambao watakuwa tayari kufanya biashara
na rapper huyo kupitia service na application yake ya kusikiliza na
kudownload muziki TIDAL… Akiwa Nigeria Bee High alifanikiwa kukutana na Don Jazzy boss wa lebo ya Mavin Records, MI Abaga boss wa lebo ya Chocolate City pamoja na P Square wenyewe.
Post a Comment