Diamond Platnumz,nilirepost Nataka kulewa ili wanigeria wajue ni mziki wa Tanzania unakubalika,alichosema kuhusu post za Swizz beats.
Jumapili ya Sept 27 2015 producer na rapa kutoka Marekani Swizz Beats aliweka kwenye instagram yake video za yeye na mtoto wake wakiburudika na nyimbo za Diamond Platnumz.
Diamond Platnumz ameongea haya machache kuhusu shavu hili la Swiz beats…
” Nilikuwa studio nikaambiwa tu jamaa kapost wimbo wake, baada ya dakika chache nikaona amenifollow ndio maana nikaweka picha nikiwa studio na Neyo ili akinifuatilia zaidi ajue jamaa niko powa sababu ya collabo za kimataifa, nilitaka kurepost Nana ila nikajua wanigeria watajua Swizz kasikiliza nyimbo kupitia Nigeria, nili repost Nataka kulewa ili kuwaonyesha wanaigeria ni muziki wa Tanzania unakubalika” .
Post za Swiss Beats za nyimbo ya za Diamond zilikuwa reposted na mashabiki wengi sana kuonyesha kufurahishwa na kitendo cha Swizz Beats.
Post a Comment