Msanii huyo alipokuta na Millardayo
aliweza kueleza sababu zilizomfanya kuendelea kusupport kampeni za
wagombea katika kipindi hiki cha Uchaguzi na kusema…‘Kiukweli
siwezi kusema ni changamoto kwangu ila naona tu kuna baadhi ya watu
ambao hawataki kukubaliana na ukweli na usawa wangu mimi na uamuzi wangu
mimi kwasababu mimi ni mtanzania ni mtu pia ambaye nataka maendeleo
kama watu wengi na ukiangalia tangu naanza wimbo wangu wa kwanza nenda
kamwambie natoa Mbagala nikaubadilisha nikaimba CCM’ – Diamond Platnumz
‘Kwa hiyo huyo ni moja kati ya wanasiasa ambaye anajalia na kudhamini mtu, ku support chama haiwezi kuchafua brand yangu kwasababu mwisho wa siku hivi vitu tunavyovifanya watu tu wataenda kupiga kura na Rais atapatikana wa Ikulu na sidhani kama mtu atapata nafasi ya kuingia Ikulu labda wasanii tu kwa hiyo hivi ni vitu tu tunaleta ushabiki kama timu za mpira’ – Diamond Platnumz
‘Kwa hiyo mtu akisema ananikasirikia mimi kisa nashabiki CCM ningependa kusema hizi ni siasa tu, kwa upande wa wasanii kuna Ney, Wolper, Shamsa hao ni marafiki zangu tena hakuna mtu asiyejua urafiki wangu na Ney hizi ni siasa tu kubishana mwisho wa siku maisha yanaendelea’ – Diamond Platnumz
Post a Comment