wenye headlines za burudani leo nimekutana na stori moja inayomhusu R&B superstaa Chris Brown ambaye kwa mujibu wa mtandao wa The Guardian inasemekana kuwa staa huyo amenyiwa Visa ya kwenda kufanya tour yake nchini Australia December mwaka huu!
Waziri wa Uhamiaji Australia, Peter Dutton ametoa sababu za kwaini Chris Brown amezuiliwa kuingia nchini humo akidai jamaa kazuiliwa kutokana na “vitendo vinavyoambatana na tabia yake” kupingwa na vyombo mbalimbali vya haki za wanawake nchini humo!
Japo kuna sababu nyingi amabazo zingepelekea Uhamiaji kuzuia kuingia kwa Chris Brown nchini Australia ila inaonekana sababu kuu ya yeye kukataliwa visa ni hukumu iliyotolewa juu yake mwaka 2009 dhidi ya kumpiga aliyekuwa girlfriend wake kipindi hicho Rihanna.
Baadhi ya vikundi vinavyopambana na vitendo vya unyanyasaji nchini Australia vimepinga kwa nguvu ujio wa Chris Brown nchini humo huku wakidai issue ya mwaka 2009 bado ina uzito mkubwa nchini humo!
Kikundi cha ‘GetUp’ kilipata time ya kuzungumza na chombo cha habari cha SkyNews na kusema kuwa issue sio Chris Brown kwenda Australia
ila issue ni vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake ambavyo msanii
huyo ana historia navyo na kitendo cha kumruhusu yeye kuja Australia itakuwa kama kuyafumbia macho vitendo hivyo dhidi ya wanawake.
Wizara ya Uhamiaji Australia imempatia Chris Brown siku 28 kukata rufaa juu ya kuzuiliwa kwake kwenda nchini humo mwisho wa mwaka, kwani tour yake ilipangwa kuanza December 9 kwenye mji wa Perth.
Post a Comment