Kabla ya dirisha la usajili halijafungwa mwezi August mwaka 2015, barani Ulaya kulikuwa
na stori tofauti tofauti kuhusiana na baadhi ya wachezaji nyota
kuhusishwa kutaka kuvihama vilabu vyao na kujiunga na timu nyingine.
Moja kati ya mastaa waliokuwa wanahusishwa kuhama timu zao ni Neymar ambaye alitajwa kuwa katika mipango ya Man United.
September 25 mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil anayekipiga katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania, amefunguka kuhusiana na mpango huo wa yeye kutaka kuhamia Man United katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August mwaka huu.
“Ni kweli
tulikuwa na mazungumzo ya awali, lakini hakukuwa na nia ya dhati katika
hili, awali nilisikia kuwa kulikuwa na ofa kwa ajili yangu lakini hakuna
kilichofanyika kwangu”>>> Neymar
Post a Comment