Ads (728x90)

Tabs

Page

Ali K 5Ni mwezi mmoja umebaki kufikia siku nyingine kubwa kwa Watanzania kupiga kura kumchagua Rais wanaemtaka, Wabunge pamoja na Madiwani kwenye Uchaguzi mkuu utakaofanyika October 25 2015.
Tayari mpaka sasa tumeona Mastaa mbalimbali wa Tanzania ambao hawajaficha hisia zao ni nani wanamkubali zaidi kwenye kumpa uongozi wa nchi na nafasi nyingine zinazogombaniwa.
basiMwimbaji staa wa bongofleva Ali Kiba ameungana na mastaa wengine kama Diamond Platnumz, Wema Sepetu, Steve Nyerere, Aunty Ezekiel, Ray ‘Vicent Kigosi’ na wengine kuiunga mkono CCM na mgombea wake Urais ambaye ni Dr. John Pombe Magufuli.
Pamoja na kwamba Ali Kiba ameonekana kwenye headlines za kampeni za CCM, hakuwahi kuandika au kupost chochote kwenye kurasa zake kuhusu kiongozi gani anaeona ni sahihi kwake ila sasa ndio amefanya maamuzi hayo kwa mara ya kwanza.
Ali Kiba aliandika kwenye page yake ya Instagram >>> ‘Chaguo langu sahihi MAGUFULI #hapakazitu #KingKiba na kisha Kiba baadae akaweka picha nyingine ya Dr. Magufuli na kuandika ‘ MAGUFULI #hapakazitu #KingKiba

Post a Comment