Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo ambaye ni baba wa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Cristiano Ronaldo Junior,
September 25 amepiga picha na kuiweka katika account yake ya Instagram
huku akiwa na tabasamu la furaha linalotafsiriwa kuwa ni furaha yake ya
kukaribia kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa Real Madrid wa muda wote.
Cristiano Ronaldo anatajwa kuwa, huenda akaingia katika rekodi ya ufungaji bora wa muda wote wa klabu ya Real Madrid endapo atafanikiwa kufunga hat trick katika mchezo wa September 26 dhidi ya Malaga katika uwanja wao wa nyumbani Santiago Bernabeu. Rekodi ya ufungaji wa muda wote kwa sasa inashikiliwa na Raul ambaye ana magoli 323.
Uwezekano wa Cristiano Ronaldo
kuvunja rekodi hiyo Jumamosi ya September 26 upo licha ya kuwa hadi
sasa amefunga goli nane katika mashindano yote kwa msimu huu ila bado
hajafunga goli lolote katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu msimu huu. Ronaldo alifunga goli tano katika mechi ya Laliga dhidi ya Espanyol na alifunga hat trick katika mechi ya UEFA dhidi ya Shakhtar Donetsk.
Post a Comment