Baada ya kusherekea miaka 26 ya uhai wake, msanii wa muziki wa HipHop kutoka Marekani, Tyga aliamua kuitembelea studio ya Power 106 Los Angeles na kupiga stori mbili, tatu. Akiwa kwenye interview na kipindi cha radio hiyo, Tyga aliulizwa mtazamo wake juu ya list ya Billboard 10 Greatest Rappers Of All Time… unajua alisemaje?
Tyga aliwaambia wasikilizaji wa Power 106 Los Angeles kuwa list iliyotolewa na mtandao wa Billboard
ipo sawa na wala haina makosa yoyote yale japo ingeleta maana zaidi
kama list hiyo ingesogezwa toka mwaka 2005 huku akisisitiza kuwa Drake na J. Cole ni rappers wawili ambao wanatakiwa wapewe heshima kubwa sana kwenye list hiyo.
>>> “List
ya Billboard haina shida na nahisi kama list yao ingetoka mwaka 2005
basi ingeleta maana zaidi kwani lazima ungetoa credit kubwa zaidi kwa
Drake, J. Cole hata Kendrick Lamar pia, japo list ilijaa watu wengi wa
zamani. Lakini kama wameamua kuitoa sasa hivi sioni tatizo kwasababu ni
jarida lao na huo ni mtazamo wao!” <<< Tyga alikiambia kipindi cha radio kwenye Power 106 Los Angeles, Marekani.
Baadaye Tyga akagusia kwenye uwezo wa wasanii kuchangia kwenye game ya muziki wa HipHop, na kuwataja watu kama Jay Z, Kanye West, Birdman na Lil Wayne kama wasanii waliochangia zaidi kwenye muziki wa HipHop kwa kuwapa wasanii wengine fursa za kujaribu ndoto zao kwenye game.
>>> “Mtu
kama Jay Z ukiangalia mambo yote aliyoyafanya nyuma kuchangia kukuza
vipaji vya wasanii unaweza ukataja njia alizotumia. Amewagundua watu
kama Kanye West na badaae Kanye akatuletea Common na Big Sean. Birdman
alituletea Lil Wayne na Juvenile na Wayne amewaleta watu kama mimi,
Drake na Nicki Minaj kwenye game. Kwahiyo mwisho wa siku swali kubwa ni
‘nani anajitoa zaidi kukuza vipaji kwenye game’ “<<< alimalizia Tyga.
Post a Comment