Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose (kulia), akizungumza kabla ya uzinduzi wa filamu hiyo.
Mwakilishi kutoka taasisi ya DFID, Jane Miller OBE (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Koshuma Mtengeti na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake wa Afya, Utafiti na Maendeleo (Forward), Naana Otoo-Oyortey MBE.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Rusimbi (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake wa Afya, Utafiti na Maendeleo (Forward),
Naana Otoo-Oyortey MBE (katikati), akichangia jambo katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Koshuma Mtengeti (kulia),
akielezea kuhusu filamu hiyo na changamoto mbalimbali za ukeketaji
nchini.
Na Dotto Mwaibale
LICHA
ya Mkoa wa Dar es Salaam kuonekana kwamba una watu wenye uelewa mkubwa
juu ya madhara ya ukeketaji lakini unaongoza kwa asilimia 38 ya
ukeketaji imeelezwa. Hayo
yalibanishwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Wizara ya Wanawake na
Watoto, Margaret Mussai Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Filamu
ya Simulizi halisi ya Ghati na Rhobi uliofanyika nyumbani kwa Balozi wa
Uingereza hapa nchini.
“Hali
ya ukeketaji hapa nchini bado ni changamoto kubwa kutokana na jamii
kutokuwa na uelewa mkubwa ikiwa ni pamoja na mila za baadhi ya makabila”
alisema Mussai.
Alisema
suala la ukeketaji limekuwa na changamoto kubwa kwa sababu ya wahusika
wanaofanya ukeketaji wanatengeneza fedha na kwa msichana anayefanyiwa
kitendo hicho anaonekana kuwa na thamani kuliko yule ambaye hajakeketwa.
Alisema
kwa mkoa wa Dar es Salaam kuna maeneo ambayo yanaongoza kwa ukeketaji
na wasichana hupenda kufanyiwa hivyo ili waonekane wenye heshima.
Alisema
mkoa wa Dar es Salaam una asilimia 38 ya ukeketaji, Mara asilimia 58,
Shinyanga asilimia 55 huku ikifuatia mikoa mingine.
Balozi
wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose filamu hiyo inawahusu
wasichana wawili ambao wanapinga ukeketaji katika jamii yao.
Alisema
wasichana hao waqnaonesha ujasiri wa kukataa kitendo hicho chenye
maumivu makali na kwa msaada wanafanikiwa kubadisha jinsi jamii yao
inavyomchukulia msichana katika kipindi chake cha mpito kutoka usichana
hadi kwenda kufikia utu uzima.
“Filamu
hii inaonesha kwamba si jamii zote ndani ya Tanzania zinazojihusisha na
ukeketaji na kwamba maeneo mengi wameamua kuachana na ukeketaji na
kuamini kwamba ukeketaji unawezwa kutokomezwa” alisema Melrose.
Alisema
mtoto wa kike ana haki ya kusomeshwa na kuendelezwa badala ya kuachwa
nyumbani na kufanyiwa vitendo hivyo vinavyodumaza jamii kimaendeleo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Koshuma Mtengeti alisema
changamoto kubwa ni sheria ya makosa ya ukeketaji kuto kuwa na meno
kwani ni mtu mmoja tu aliyehukumiwa kati ya watu 43 waliobainika na
makosa hayo.
Filamu
hiyo imeandaliwa na ubalozi huo kwa kushirikiana na Jukwaa la Utu wa
Mtoto (CDF) na Mfuko wa Wanawake wa Afya, Utafiti na Maendeleo
(Forward).
Post a Comment