Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger ni
miongoni mwa makocha wanaotajwa kuwa wagumu wa kutumia fedha nyingi
katika kuwekeza kununua wachezaji na kuboresha kikosi chake, Wenger
mara nyingi majina ya wachezaji wakubwa na wanaouzwa kwa gharama za juu
huwa anashindwa kuwasajili na mwisho wa siku wanasajiliwa na timu
nyingine.
November 25 kauli ya kocha wa Arsenal Arsene Wenger
imeingia katika headlines baada ya kuulizwa swali na muandishi kutokana
na mwenendo wa tabia yake ya matumizi ya fedha hususani tukiwa
tunaelekea katika dirisha dogo la usajili la mwezi January, hakubaliani
na watu wanaomuita yeye bahili.
“Hapana
sikubaliani na wewe kuwa mimi mbahili kama nitapata nafasi ya kukutoa
out ndio utakapojua namna ambavyo huwa napenda kutumia fedha, rafiki
zangu huwa hawanifirii hivyo, kwa sasa tunaenda kucheza na Olympiacos na
tunaamini tutafuzu hatua ya 16 bora ya UEFA” >>> Arsene Wenger
Wenger
usiku wa November 25 alifufua matumaini ya kikosi chake kusonga mbele
katika michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya baada ya kufanikiwa
kuifunga klabu ya Dinamo Zagreb kwa jumla ya goli 3-0,
hivyo matumaini ya kwenda hatua inayofuata yapo endapo watafanikiwa
kushinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya Olympiacos.
Video ya Arsene Wenger akijibu kuhusu stori za yeye kuitwa mbahili
Post a Comment