Ads (728x90)

Tabs

Page

Mkemia Mkuu wa Serikali Samuel Manyele leo amekutana na waandihi wa habari katika ofisi yake, Dar es salaam na kuzungumzia suala zima la kemikali hatarishi zinazoingia nchini kinyume na sheria pamoja na mikakati waliyojiwekea.
Sheri  za kuingiza kemikali nchini..“Kila mtu anayetaka kuingiza kemikali nchini lazima apate kibali na kuhakikisha kwamba ni salama kwa afya za wananchi..tumetayarisha muongozo kwa watendaji wa bandari ili kushughulikia kemikali hatari na utasambazwa kwa wadau kabla ya kuanza kutumika”.
“Tumeanzisha bandari kavu kwa ajili ya kuhifadhi kemikali hatarishi na kusimamiwa kabla ya kuanza safari ya kwenda kwenye nchi kavu..kuhakikisha viwango vimezingatiwa., utaratibu huu utarahishisha usimamizi wa kukabiliana na madhara yoyote yatakayoweza kujitokeza”..Prof. Samuel Manyele
Kiasi cha kemikali zilizoingia nchini tangu Januari hadi oktoba 2015..“Jumla ya tani zilizoingia kwenye mipaka mbalimbali na bandari jumla ya tani 472,393 za Kemikali ziliingizwa nchini kwa kipindi cha miezi kumi, bandari ya Dar es salaam ndio inaongoza kwa kuwa na tani nyingi 281,468 ikifuatiwa na Tunduma yenye tani 199, 000, Mtwara, Tanga, Horohoro, Mwanza na Sirari…tuna list kubwa inayoonyesha ni kiasi gani kemikali hizo zinapita katika bandari hizo”...Prof. Samuel Manyele
Mpaka wa Tunduma unapitisha Kemikali nyingi kutoka Tanzania kwenda nchi za nje na ni 80% ya kemikali hupita katika bandari hiyo..
Pia amezungumzia mikakati ya Serikali..”Kuongeza watumishi kwa wakala ambao wameanza kupelekwa kwenye mipaka inayoingiza kemikali kwa wingi, kuiwezesha Serikali kufuatilia kemikali hizo kwa ukaribu, Serikali kufanya maamuzi ya ajira kiasi gani zitolewe na tayari watumishi wameanza kusambazwa katika mipaka yote inayoingiza Kemikali hizo”..Prof.Samuel Manyele
Vibali vinatolewaje?..“Kuna kemikali ambazo ni hatari sana kwa binadamu na haziruhusiwi kuingia nchini..”Hutolewa kwa matumizi ya Serikali tu”.

Post a Comment