Ads (728x90)

Tabs

Page

Msanii Shilole aliwai kuingia kwenye headlines baada ya ku-post kwenye instagram picha ya nyumba yake ambayo alikua bado anaijenga. Caption ya picha hiyo ilikua inasomeka hivi, “Mungu nisaidie nimalize hii kitu ili watoto wangu wasije kupata tabu”.
Eneo ambalo alilokua anajenga nyumba hiyo ni Kimara jijini Dar es Salaam lakini Shilole amesema kwamba ameuza nyumba hiyo ambayo ilikua bado haijaisha vizuri.
Akiongea na millardayo.com Shilole ametoa sababu za kuuza nyumba hiyo kama hivi, “Nyumba yangu niliyokua naijenga maeneo ya Kimara nimeiuza kwenye hatua iliyofikia kama ilivyokua inaonekana kwenye picha. Sababu ya msingi iliyonifanya kuiuza ni kwamba pale eneo nililokua najenga ni nimegundua kwamba ni njia ya maji. Hivyo basi sitaki kupata tabu msimu wa mvua ukianza maji yakiwa yanapita nje ya nyumba yangu. Pia hakuna tatizo nimeuza nitajenga kwingine mambo ni mazuri”
Shilole wiki hii ametoa wimbo mpya unaitwa Nyan’ganyan’ga produced by Mazuu Records.
Hii ndiyo nyumba yenyewe

Post a Comment