Baada ya kutembelea studio za HOT 97 na kufanya kipindi cha asubuhi cha Ebro In The Morning, Chris Brown alizitembelea pia studio za Power 106 kwa ajili ya kufanya kipindi kingine na Angie Martinez na kupiga nae stori nyingi ikiwa na kuongelea Album yake, mapenzi na mipango yake ya Christmas kwa mwaka huu.
Kikubwa alichokigusia Chris Brown kwenye show ya Angie Martinez ni sababu za kwanini akishirikishwa kwenye single ya msanii huwa hadai pesa yoyote! Yes mtu wangu, amini usiamini Chris amesema hana mazoea ya kudai pesa ya kazi alizoshirikishwa! Kwanini? Ipokee hii kutoka kwake…
>>> “Huwa
sipendelei kuchaji pesa kwa kazi za wasanii nilizoshirikishwa kwa
sababu kwanza ninaandikia wasanii wengi na wengi ninaoshirikishwa kwenye
ngoma zao mara nyingi unakuta alishawahi kunisaidia kwenye wimbo wangu
kwahiyo anapokuja kwangu na mimi narudisha favor hiyo…” <<< Chris Brown.
Sasa Chris Brown anapataje hela kwa kazi za kushirikishwa?: >>> “Hela
ninayopata kwa kazi kama hizo ni ile asilimia yangu ya mauzo
inayotokana na wimbo kuingia sokoni na kuuza, kwa sababu pia huwa
naandika mashairi yangu, so kama nimechangia mashairi basi napata
asilimia yangu pia“. <<< Chris Brown.
Chris
aliogezea kuwa hapendi kulipwa pesa kwa kazi za kushirikishwa kwa
sababu anachoangalia sana kwenye kazi hizo ni ule uhusiano alionao kati
yake na msanii husika na kama mtu huyo ni miongoni ya watu wake wakubwa
basi hana haja ya kuwadai kwasababu anachokilinda zaidi ni ule uhusiano
wake na mtu huyo na sio ule mshiko wa pesa.
>>> “Ila
sio kwamba sidai kabisa pesa hapana, inategemea na mtu na uhusiano
nilionao na huyo mtu… lakini kwa wasanii wa underground lazima
nitangulize bei yangu ya biashara kwani pale nitakapoamua kukubali
kushirikishwa kwenye ngoma ya underground basi jua ngoma hiyo
itamtambulisha msanii huyo kwenye game… na ni muhimu kulinda brand yako
ukiacha hayo yote” <<< Chris Brown.
Post a Comment