Nimepata stori kutoka Uingereza masaa kadhaa yaliopita, ambako mchezaji maarufu wa Tennis duniani Serena Williams anaziandika headlines za leo kwenye ukurasa wa michezo.
Serena Williams leo amecheza mechi ya mwisho ya Tennis ya Sixth Wimbledon Singles Title na ameibuka kidedea baada ya kumshinda mpinzani wake Garbine Muguruza. Ushindi huu ni wa nne kwa mfululizo kwa Serena.
Kizuri zaidi ni kwamba ushindi wa aina hii unamuweka
Serena Williams kwenye nafasi ya kucheza mechi za U.S Open na kama akishinda mechi hizo Serena atakuwa mwanamke wa kwanza kushinda mechi hizo toka Steffi Graf achukue ushindi mwaka 1988.Akiwa na miaka 33 tu Serena Williams anahesabika kama mwanamke mwenye umri mkubwa kushinda Grand Slam Title. Mpaka sasa anashikilia ushindi wa major championships saba, na baada ya ushindi huu Serena sasa anashikilia Grand Slam Titles 21.
Post a Comment