Kingunge
aliyejitoa kindakindaki kumpigania mbunge wa Monduli na waziri mkuu wa
zamani Edward Lowassa, amekuwa akitoa matamko mbalimbali kuhusiana na
mchakato huo na zaidi akisema haukutenda haki hasa baada ya kuenguliwa
jina la Lowassa.
Kamati ya Usalama na Maadili, Kamati
Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa, ndizo zilizokuwa na kazi ya kuchuja
majina hadi kupatikana mgombea mmoja, Dk John Magufuli.
Akizungumza
jana kwa simu kutoka Bumbuli Tanga, Makamba (pichani) alisema: “Mzee
Kingunge ni mtu mzima, ninamuheshimu sana, ni mkongwe katika siasa,
lakini anakivuruga chama.”
Alisema binafsi hakubaliani
na kauli za Kingunge kupinga uteuzi wa Dk Magufuli kwa sababu makada
wote wa chama waliokuwapo Dodoma, waliamua kumpitisha kwa kuwa walimuona
anafaa na anaweza kukijenga chama.
“Ndani ya chama
kuna wazee wenye busara ambao waliangalia vitu vingi hadi kumteua
mgombea kwani unaweza kuwa mtendaji mzuri lakini ukawa na kasoro nyingi
hivyo, unaweza vilevile kuonekana ukashindwa kukivusha chama kwenye
ushindi.
“Mimi ninamuheshimu sana Mzee Kingunge, lakini
siwezi kukubaliana naye anavyokandia mchakato. Mimi ninaamini ulikuwa
sahihi, kila mtu ameridhika na ndiyo maana kura zilipigwa…, tuna imani
naye na anaweza kuongoza tangu zamani,” alisema Makamba.
Makamba
alisema, ana imani kwamba atafanya vizuri hivyo ni bora apewe
ushirikiano kama walivyopewa viongozi waliopita ili kukinusuru Chama cha
Mapinduzi na watu waendelee kukiheshimu kama awali.
Katibu
mkuu mstaafu wa chama hicho, Yusuph Makamba alikaririwa na vyombo vya
habari juzi akisema kwamba, watu wanaoendelea kulalamikia mchakato wa
kumpata mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk Magufuli wana masilahi
binafsi na siyo kwa ajili ya kukiimarisha chama hicho.
Kauli ya Kingunge
Akizungumza
na waandishi wa habari nyumbani kwake mwanzoni mwa wiki, Katibu huyo wa
zamani wa halmashauri kuu ya CCM alisema, Kamati ya Usalama na Maadili
iliteka majukumu ya Kamati Kuu baada ya kuamua kuchuja majina ya makada
waliojitokeza kuwania urais hadi kufikia watano, akisema jitihada hizo
zilifanywa kwa kuvunja kanuni na zililenga kumuengua Lowassa kuwania
kuingia Ikulu.
Kingunge alisema kitendo cha kumuengua
Lowassa kwa kuvunja kanuni kimeacha kasoro kubwa ndani ya chama hicho
tawala kwa sababu taratibu zilikiukwa ili kupata viongozi.
Alisema
kosa hilo siyo la Dk Magufuli aliyepitishwa kuwa mgombea urais wa CCM,
na wala si la Lowassa, bali ni la waliopendekeza majina ya walioingia
tano bora.
Jina la Lowassa, ambaye alijidhihirisha
kukubalika ndani na nje ya CCM kutokana na harakati zake za kusaka
wadhamini kujaa watu, halikupelekwa kwenye Kamati Kuu, kwa mujibu wa
Kingunge na hivyo kutojadiliwa na chombo hicho ambacho kilimpitisha Dk
Magufuli, Dk Asha-Rose Migiro, January Makamba, Bernard Membe na Balozi
Amina Salum Ali
Post a Comment