Sakata la usajili wa beki wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Real Madrid, Sergio Ramos leo asubuhi limechukua nafasi tena kwenye headlines za vyombo habari ulimwenguni kwa ishu nyingine tena.
Ramos ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akihusishwa na kujiunga na Manchester United, amegoma kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Real Madrid.
Ila wakati kukiwa na taarifa kwamba United inajiandaa kutuma ofa mpya ya paundi millioni 42 kwenda Madrid, leo hii asubuhi kocha mpya wa Real, Rafael Benitez amesema kwamba mchezaji hatohama katika klabu hiyo msimu.
Benitez ameyaongea haya mbele ya waandinshi wa Habari leo >>>> “Sergio
yupo katika sehemu muhimu ya timu yangu, ni mshindi ni aina ya
wachezaji wa namna hiyo tu ndio tunaohitaji… Ninachojali mimi ni kauli
ya Rais kwamba mchezaji huyu atabaki kwenye klabu hii, nimeshaongea na
Ramos kwa kirefu kuhusu hatma yake na mawazo yake“>>>>
Post a Comment