Akizungumza na Clouds E ya Clouds TV, Nay amesema bado kuna video zinakuja zitakazokuwa na damu.
“Hii ni video ya pili naifanya hivi na kutakuwa na video nyingine ya
tatu ambayo itakuwa na vitu kama hivyo,” alisema. “Hii ni kama sign
yangu, kwahiyo nimepokea maoni mengi kuhusu kufanana kwa hii video
lakini yote ni kwaajili ya damu na damu ni kama nilivyosema hii ni sign
yangu,” aliongeza.
Pia Nay alieleza sababu iliyofanya wimbo wake na Diamond, Mapenzi au Pesa kufeli.
“Ndio haujafanya vizuri lakini tukumbuke wimbo Mapenzi au Pesa ni wimbo
ambao umekosa video. Kwenye muziki wetu wa siku hizi watu wanataka video
haraka, ukichelewa kufanya video wimbo unakuwa unapungua kasi siku hadi
siku. Tumeshaona hili kwenye nyimbo nyingi sana za wasanii wetu,
ukichelewa kutoa video, wimbo unakufa haraka sana, yaani unakuwa
unapungua nguvu siku hadi siku.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment