Utafiti mpya umebaini kwamba mbu hutafuta kitu cha kula kwa kutumia vigezo vitatu,harufu,macho na joto.
Utafiti huo unasema kuwa mbu anaweza kufahamu aliko mwanadamu kupitia hewa ya kaboni ambayo watu hupumua nje.Inasemekana mbu hunusa hewa hii kiasi cha mita 50.
Wanasayansi wamesema kwamba walimfuatilia mbu mwenye njaa, ndani ya mtaro uliofunikiwa.
Kisha waligundua kwamba mbu hao walianza kunusa nusa hewa ya kaboni, na kutema mapovu yenye matone meusi yaliowekwa na watafiti hao sakafuni.
Imebainika kwamba wakati mbu yuko mita chache karibu na kile anacholenga, huvutiwa sana na joto.
Hii imebainisha kwamba hata hufuata joto hilo na kisha kumshambulia mwanadamu.
Huenda ukapata Malaria au ukaponea lakini utakua na vipele pale vya mbu anapokuuma.
Post a Comment