Ads (728x90)

Tabs

Page


Klabu ya Manchester City imemsajili kiungo wa Aston Villa Fabian Delph kwa mkataba wa miaka mitano… Delph amejiunga na Manchester City  ikiwa ni siku kadhaa zimepita toka atangaze kuwa hana mpango wa kuihama klabu hiyo baada ya kuhama kwa mshambuliaji Christian Benteke na kujiunga na Liverpool.

Delph amesajiliwa kwa ada ya uhamisho ya pound million 8 na anategemea kusafiri weekend hii kwenda Australia kujiunga na kikosi cha Man City kwa maandalizi ya msimu mpya.
Delph akionesha uzi aliokabidhiwa, namba 18 mgongoni Man City.
Delph alisaini mkataba wa miaka minne na Aston Villa miezi sita iliyopita baada ya ule wa awali kukaribia kumalizika na amecheza mechi 28 za Ligi kuu Uingereza akiwa na Aston Villa na mchezo mmoja wa fainali ya kombe la FA.

Post a Comment