Ads (728x90)

Tabs

Page

Baada ya kuachia album yake iitwayo ‘1989’ msanii wa muziki wa Pop R&B nchini Marekani, Taylor Swift amekuwa akiweka headlines nyingi sana kuanzia kwenye ushindi wa tuzo na pia hata kwenye rekodi za shows, na kwenye tour zake nyingi amekuwa akiwaalika wasanii tofauti kuja kuperform nae jukwani… Lakini itakuaje pale ambapo Rihanna ataombwa kwenda kufanya show na Taylor Swift!?
riri2
Rihanna na Taylor Swift.
Rihanna amewaacha watu hoi baada ya kauli aliyoitoa kwenye interview aliofanya na NME UK Magazine kuwaacha watu na maswali mengi kichwani… Akiwa kwenye interview hiyo Rihanna aliulizwa anaonaje kwenda tour na kushare stage moja na Taylor Swift… jibu la Rihanna lilikuwa hili hapa;
>>> “Sidhani kama nitaenda nae kwenye tour yake wala kuperform nae kwenye stage moja hata akinialika… Sidhani kama italeta maana yoyote kusema kweli. Sidhani pia kama brand zetu ziko levo moja na wala sidhani kama zinafanana, na pia sidhani kama mashabiki wetu wako sawa!” <<< Rihanna.
riri4
Rihanna.
Kauli hii iliwaacha watu wakiwa na maswali mengi sana, baadhi wakijiuliza je Rihanna na Taylor Swift wana ugomvi wowote ama hili ni beef la chini chini!?… Lakini Rihanna alipoulizwa kwenye interview ya pili staa huyo wa BBHM alikuwa na haya ya kusema…
taylor swift
Taylor Swift.
>>> “Hapana… nilisema hivyo kwa sababu Taylor sasa hivi ni msanii mkubwa sana, mwaka jana na mwaka huu Taylor amepata mafanikio makubwa sana na ana mashabiki ambao naamini ni wengi zaidi kushinda wangu, nilisema yote yale sio kwa ubaya na wala sina tatizo na Taylor… isitoshe nampenda sana Taylor, yule ni “role model wangu” mkubwa sana… sema tu nahisi Taylor ni maarufu zaidi kushinda mimi ndio maana niliongea vile!”<<< Rihanna.
Kumbe issue ni Taylor Swift kumzidi umaarufu Rihanna! Je wewe unaonaje mtu wangu, kati ya Rihanna na Taylor Swift nani ni maarufu na mwenye mashabiki wengi zaidi!?

Post a Comment