Huenda ukawa umesikia stori nyingi kuhusu Dubai ila hii ikawa ilikupita, Dubai ni moja kati ya sehemu zinazoongoza kuwa na majumba ya kifahari hoteli nzuri, karibia kila kitu kilichomo ndani ya Dubai ni kivutio kwa wageni kutoka nchi nyingine, hata gari za polisi za Dubai ni gari ambazo za thamani kubwa.
Ni kawaida kwa Dubai kuona Ferrari, Lamborghini na
magari mengine ya kifahari kutumika kama magari ya polisi wakati kwa
nchi nyingine hutumiwa na watu matajiri sana na wenye kipato kikubwa.
Sasa hii ni stori nyingine tena ya kuvutia kutoka Dubai kuhusu mchezo wa tennis.
Dubai ndio sehemu pekee
kuna uwanja wa tennis mrefu kuliko yote wa kuvutia, mrefu kwa maana
umejengwa juu ya ghorofa, ila stori sio tu kuwa juu ila ni namna ambavyo
umejengwa katika hoteli inayotajwa kuwa ya nyota saba duniani Burj Al Arab.
Post a Comment