Akiongea na waandishi wa habari, msemaji wa jeshi la polisi, Advera Bulimba..’Katika
kipindi hiki knachoendelea cha kampeni hali ya usalama inaonekana ni
shwari hakuna matukio makubwa ambayo yaliyoripotiwa yakushtua
tunawashukuru wananchi lakini pia viongozi wa vyama vya siasa na wafuasi
wao ambao wamekuwa wakitii sheria za nchi’ – Advera Bulimba
‘Hata hivyo pamoja na ushwari huo bado
kumejitokeza baadhi ya watu wachache kufanya vitendo vya uhalifu vyenye
mweleko wa kuvunja amani ambayo hata hivyo wameweza kuthibitiwa na jeshi
la polisi jumla ya matukio 107 yameripotiwa katika vituo vya polisi
kati ya matukio hayo matukio 38 tayari yamefunguliwa kesi na kufikishwa
mahakamani’ – Advera Bulimba‘Hayo matukio 38 ambayo yafunguliwa kesi na kufikishwa mahakamani yana jumla ya watuhumiwa 52 ambao tayari tumewafikisha mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake, aidha matukio mengine yaliyobaki 68 bado yapo chini ya upelelezi wa jeshi la polisi, katika matukio hayo ambayo tumeyafikisha mahakamani wengi wanatuhumiwa kuvunja kufanya makosa yafuatayo ikiwemo wafuasi wa chama kimoja kuvamia ama kuzomea wafuasi wa chama kingine hususani wanapokuwa katika kampeni za uchaguzi maeneo mbalimbali ya mikoani‘ – Advera Bulimba
Post a Comment