Miongoni mwa sehemu nzuri na zakuvutia kutembelea katika hii Dunia basi Dubai haiwezi kukosa, Dubai
unatajwa kuwa mji wa kitalii na kibiashara, wengine wanautaja kama pepo
ya watalii. Mji huo umejengeka kwa majengo yenye ramani za kuvutia.
September 17 nakusogezea list ya maajabu 15 ya Dubai stori kutoka worldtoptop.com.
Hadi kufikia June 2013 hizi ni sehemu 10 zilizokuwa zinatajwa kuwa nzuri na zakuvutia Dubai.
-
Burj al Arab
Burj
al Arab ni hoteli yenye hadhi ya nyota 7 ina vingi vya kuvutia, ikiwa
ni pamoja na kuwa na uwanja wa tennis ulio juu, mgahawa chini ya bahari.
Lakini Burj al Arab ni moja kati ya hoteli zinazoitambulisha Dubai.
2-Visiwa vya Palm
Visiwa
vya Palm ni visiwa vikubwa zaidi vilivyotengenezwa na binadamu sio
visiwa vya asili kama ilivyo kwa Zanzibar na vingine, visiwa hivyo
vinatajwa kuwa miongoni mwa maajabu 8 ya Dunia.
3.
Burj Khalifa
Burj Khalifa inatajwa kuwa jengo refu Duniani lililojengwa na binadamu, Burj Khalifa ni jengo lenye ghorofa 160.
4.
Dubai Marina
Dubai
Marina ni mfereji mkubwa zaidi Duniani uliojengwa na binadamu, Dubai
Marina una sehemu za kupaki boti ndogo lakini ni mji ambao umetengenezwa
kuweza kuchukua watu 120000.
5.
Infinity Tower
Infinity Tower ni jengo refu lililojengwa katika mfumo wa nyuzi 90 na lina urefu wa futi 1000 kutoka chini.
6- Dubai Mall
Dubai
mall ni mall yenye eneo kubwa duniani na ina hifadhi ya wanyama ya
kutengeneza, ina vyumba 250 vya Luxury hoteli lakini ina chem chem.
7.
Jumeirah Beach Hotel
Jumeirah Beach Hoteli ni hoteli yenye hadhi ya nyota 5 , ramani yake ni kama wimbi la maji ya bahari.
8.
Dubai Fountain
Hii ni chem chem iliyopo Dubai kama hufahamu chemchem ni maji yatokayo ardhini lakini yanatoka yakiwa na presha.
9.
Atlantis The Palm Hotel & Resort
Atlantis
The Palm Hoteli & Resort ni hoteli yenye vyumba vya kulala chini ya
maji ambapo ukilala katika hivyo vyumba unaweza pata nafasi ya kuona
samaki wakubwa kama papa na wengineo.
10.
Ski Dubai
Ski
Dubai ni sehemu yenye theluji ina ukubwa wa mita za mraba 22500,
inatumika kama sehemu ya kuenjoy kwa baadhi ya michezo ambayo huchezwa
sehemu kama hizo.
Post a Comment