Na Salym Juma
Claudio Ranieri ameanza kutajwa
sana kama Meneja aliyerejea kwa kasi kwenye EPL na kuanza kutishia uhai
wa timu ndogo ambazo ziliamini Leicester City na Sunderland ndio wahanga
wa kuteremka daraja hivo wao hawatokuwa na shaka kumbe sivyo. Leicester
wameanza vyema na uwezo wao unachagizwa na kiwango kikubwa cha kijana
mmoja wa kiarabu ambaye alionekana kwenye kombe la dunia pale Brazil.
Kijana huyu amekuwa sio anatoa assist pekee bali anafunga magoli
yanayoihakikishia timu yake uhakika wa pointi 3. Leo naomba tumtazame
Riyad Mahrez,winga ambaye ndiye anayekusudiwa hapa.
Alitumia muda mwingi kucheza
kwenye timu ya vijana ya mtaani kwake ya AAS Sarcelles kabla ya mwaka
2009 kuanza kucheza soka la kulipwa kwenye timu ya Quimper, kwa sasa
timu hii ipo ligi daraja la 4 pale Ufaransa. Pia Le Havre ambayo ipo
French Legue 2 ilimchukua na hapa ndipo Leicester City walipomuona na
kumpa kandarasi ya kudumu. Akiwa Ufaransa Mahrez alitupia magoli 32
katika michezo 147 huku akitengeneza magoli ya kutosha kwa washambuliaji
wa timu alizopitia.
Mahrez alianza kuonesha makucha yake tangu Leicester ikiwa chini huku
akiwa miongoni mwa walioipandisha timu hii daraja.
Mahrez alianza kuonesha makucha yake tangu Leicester ikiwa chini huku
akiwa miongoni mwa walioipandisha timu hii daraja.
Magoli 4 aliyoyafunga kwenye
mechi za ufunguzi na kiwango chake cha kutisha, vimemfanya atajwe
kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi. Sio rahisi kuaminiwa na kutajwa
kwenye tuzo hii kwani kuna wachezaji wenye viwango vikubwa kwenye EPL.
Japokuwa tuzo hii ilichukuliwa na kijana kutoka Ghana, ila naamini
Mahrez naye alistahili kuingia kwenye kinyang’anyiro.
Mwazo wake mzuri unefanya jina
lake kuongeza umaarufu na hata Ufaransa kujuta kwanini hawakumuita
kwenye timu yao ya vijana kipindi cha nyuma kwani kwa sasa wangekuwa na
‘Asset’ ya uhakika kwenye taifa lao.Kiwango kikubwa walichokionesha
Algeria kwenye michuano ya kombe la dunia iliyopita kilichagizwa na
viwango vikubwa vya Wa-algeria akiwemo Riyad Mahrez.
Kutokana na uwezo wake wa kupiga
vyenga na kasi ya kutisha kule pembeni, ni jambo la kheri kwa kijana
huyu kwani amekuwa ni miongoni mwa wachezaji 5 katika zile ligi kubwa
ambao wanaongoza kwa kufanya ‘Dribbles’ mara kibao. Baada ya Lionel
Messi, Neymar, Alejandro Gomez na Serey Die wa Stuttgart, Mahrez ndiye
anayefata akiwa na wastani wa ‘kudribble’ mara 4.4 kwa kila mechi.
Hakuna mchezaji mwingine kutoka EPL mbali na Mahrez.
Kutokana na kiwango na mwenendo
wake ni wazi kuwa Riyad Mahrez anaelekea pazuri na huenda jina lake
likawa kubwa pale Algeria na kuwafunika akina Nabeel Bentaleb, Islam
Sliman na Yacine Brahimi. Nina wasiwasi msimu ujao Mahrez anaweza
kulihama jiji la Leicester na kwenda kutafuta maisha katika vilabu
vingine vikubwa kidogo tofauti na Leicester city. Pia usishangae kuona
anachukua tuzo za mwezi kibao kwenye EPL au hata zile za ndani ya klabu
yake. Pia tuzo za nyota wa mchezo hazitoacha kumuangukia kama atakuwa na
mwenendo huu wa kuridhisha.
Post a Comment