Ads (728x90)

Tabs

Page

Toure
Kiungo wa klabu ya Manchester City ya England na timu ya taifa Ivory Coast Yaya Toure metwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika inayotolewa na Shirika la Utangazaji nchini England (BBC) kwa mwaka 2015.
Toure anaingia kwenye orodha ya wachezaji watatu ambao wamewahi kutwaa tuzo hiyo mara mbili akiungana na Nwanko Kanu pamoja na Jay-Jay Okocha (wote wa Nigeria) ambao waliwahi kutwaa tuzo hiyo mara mbili.
Nyota huo wa Ivory Coast amesema anajivunia kuwa mshindi wa tuzo hiyo ambayo mshindi hupatikana kwa kupigiwa kura na mashabiki.
“Najivunia sana. Kupokea tuzo hii kutoka kwa mashabiki siamini”., Toure ameiambia BBC Sport.
Yaya Toure amewashinda Yacine Brahimi (Algeria), Pierre-Emerick Aubameyang (Gagon), Andre Ayew (Ghana) na Sadio Mane (Senegal) ambao walikuwa wakiwania tuzo hiyo kwa mwaka 2015.

Post a Comment