KILICHOMKUTA BENZEMA TIMU YA TAIFA ANAKIJUA MWENYEWE
Nyota wa Real Madrid Karim Benzema amepigwa stop kuchaguliwa kwenye timu ya taifa ya Ufaransa hadi pale uchunguzi wa sakata lake linalohusisha kutaka kuvujisha video ya ngono inayomhusu Mathieu Valbuena utakapokamilika, Rais wa shirikisho la soka la Ufaransa Noel Le Graet amethibisha.
“Kuanzia leo, Benzema hatakiwi kuchaguliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa”, Le Graet aliwaambia waandishi wa habari.
“Ninafahamu mtasema, lakini ni kipindi cha Christmas hivyo hakuna mechi, lakini zitakuwepo mwezi March”.
“Kama hakutakuwa na mabadiliko yoyotwe mwezi March (ambapo kutakuwa na mechi za kimataifa) hatocheza. Mtasema lakini kuna michuano ya Euro na mnampenda mchezaji huyu, hiyo itawavunja mioyo”.
Ufaransa itacheza na Uholanzi mchezo wa kirafiki wa kimataifa 25 March, 2016.
Post a Comment