Ads (728x90)

Tabs

Page

Rapper kutoka kundi la muziki la Cash Money Records, Drake ni miongoni ya wasanii waliofanikiwa kuingia kwenye nominations za The 58th Grammy Awards akiwa anawania vipengele kadhaa, baadhi vikiwa Best Rap Performance na Best Rap Song.
HLB1
Lakini kitu kimoja kilichowashtua mashabiki wengi wa Drake ni kitendo cha Tuzo za Grammy kutokuweka latest single ya Hotline Bling kwenye kipengele chochote ikiwa ni wimbo uliouza zaidi kuliko diss track ya ‘Back to Back’ na single ya ‘Energy’.
HLB2
Mtandao wa Hits Daily Double umeripoti kuwa kitendo cha Tuzo hizo kutokuuweka wimbo huo wa Drake kwenye kipengele chochote za Grammy ni tatizo lililotokana na lebo ya Drake, Cash Money Records. Mtandao huo umesema wimbo wa Hotline Bling haukutumwa na management ya Cash Money kwa The Grammys na kama lebo ya msanii huyo ingepeleka wimbo huo bila shaka wimbo wa Hotline Bling ungechaguliwa kwenye vipengele tofauti ikiwemo ‘Record of The Year’.
HLB4
Single ya Hotline Bling ilikaa kwa wiki 5 mfululizo kwenye chati ya Billboard 200, Marekani na kushikilia nafasi ya 2 kwa wiki zote hizo.

Post a Comment