Bunge la Jamuhuri ya Muungano Tanzania
litaanza muda sio mrefu baada ya Uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 2015
kukamilika… kuna mambo ya kujibizana kwa hoja, hiyo ni kawaida… lakini
kuna wakati tulishuhudia mambo yakibadilika, utata unaibuka watu
wanajibizana mpaka wanataka kushikana !!
Ugomvi ni kitu kingine ambacho kimewahi kushuhudiwa kwenye Mabunge mengi, ninayo hii ya Ukraine… Waziri Mkuu wa Ukraine, Arseny Yatsenyuk alikuwa amesimama mbele akiendelea na kuhutubia Bunge, Mbunge mmoja wa upinzani akamfuata na kumpa shada la maua.
Basi ile baada ya Waziri Mkuu
kupokea tu hilo shada, jamaa alimbeba juujuu na kumwondoa kama
anampeleka nje ya Bunge hivi… utata ukaanzia hapo, malumbano yakaendelea
huku Wabunge wa chama tawala wakimgeuzia kibao Mbunge huyo na kuanza
kumpiga.
Post a Comment