Headlines za staa wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo
kama ataendelea kuitumikia klabu hiyo au ataihama izmechukua nafasi.
Sababu kubwa zinatajwa ni namna mwenendo wa timu yake ulivyo sasa, wengi
wamekuwa wakisema hana mahusiano mazuri na kocha Rafael Benitez na sababu zingine kibao zikijumuishwa.
Kocha wa Paris Saint Germain, Laurent Blanc, hivi karibuni alionekana akiongea na Staa huyo wa Madrid, wakati walipokutana kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya (UEFA), kitendo ambacho kinatafsiriwa kama yalikuwa ni mazungumzo ya Blanc kumshawishi mchezaji huyo kuhama. Ronaldo amebakiza mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Real Madrid.
“Watu
wameshazoea jina langu na mara nyingi wamekuwa wakilihusisha kwenye aina
ya tetesi hizo, lakini timu hii imenisaidia sana tangu niwasili hapa,
nina furaha kuwa na Madrid. Kilichotokea kati yangu na Blanc ni cha
kawaida sana, kama mtu anakujali unapaswa kuwa mwema kwake. Kama kuna
mtu anayetokea Chelsea, Manchester United au Barcelona mwenye utu
hatokuwa na tatizo kwangu na naweza kuongea nae, lakini haina maana kuwa
nitajiunga na PSG, kwani bado nina mkataba na Real Madrid”
>>>> Ronaldo.
Post a Comment