Tukiwa tumemaliza headlines za Uchaguzi
Mkuu 2015, mwigizaji Frank alijitokeza kugombea Ubunge jimbo la Tabata
Segerea kupitia tiketi ya ACT-Wazalendo lakini kutokana na kura zake
kuwa chache hakufanikiwa kuwa mshindi wa jimbo hilo.
Akiongea na ripota wa millardayo.com mwigizaji huyo alisema…’Nilikuwa
mgombe ubunge jimbo la Segerea kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, ingawaje
sikuwa mshindi lakini naimani wamempokea vizuri mshindi Bonnah Kaluwa…!
Na nimekubali matokeo’– Frank
‘Bado
naonekana nina deni kwa wale walionipigia kura kama wawakilishi wa wana
Segerea, hivyo kuna baadhi ya mambo yaliyo ndani ya uwezo wangu
nitayafanya kwa wananchi wangu‘- Frank
‘Kulikuwa
na changamoto nyingi, ingawa najipanga upya mwaka 2020 kugombea tena…!
Ili kuweza kusaidi matatizo kama tatizo la maji, ujasiriamali, ajira,
michezo na afya‘-Frank
Post a Comment