Mara ya mwisho umenunua Album ya Akon ilikuwa lini?! Amini, usiamini imepita miaka saba toka Akon aziandike headlines kwenye kurasa za burudani! yes, miaka saba toka Akon aachie Album yake ya mwisho!
Good news mtu wangu, kama wewe ni miongoni wa watu wanaomkubali Akon kinoma basi ipokee hii popote pale ulipo… msanii huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa lebo yake ya Konvict Music hivi karibuni amekuwa studio akikamilisha mzigo mpya wa Album uliopewa jina ‘Stadium‘.
Kizuri zaidi ni kwamba weekend hii msanii huyo wa Pop R&B kutoka Marekeani anaisogeza kwetu single mpya kutoka kwenye Album hiyo, wimbo unaitwa ‘Whole Lot’ na ndani rapper Migos kashirikishwa.
Kama bado mdundo huu haujagusa masikio yako, basi karibu uisikilize ngoma hiyo hapa chini kwa kubonyeza play.
Post a Comment