Kitendo cha Sheria za China kupiga
marufuku watu kuzaa mtoto zaidi ya mmoja, ilikuwa ni kitu ambacho
Mataifa mengi Duniani yalikuwa yakikipiga vita, good news kutoka huko
ninayo, mambo yamebadilika japo kwa wengine wanasema bado haitoshi !!
Kwa sasa China ina jumla ya watu Bilioni
1.3 kutokana na Sera ya kila wanandoa kutakiwa kuwa na mtoto mmoja tu,
lakini Serikali ya China imeona umuhimu wa utaratibu huo kubadilishwa
ambapo kwa sasa wako wanandoa wanaruhusiwa kuwa na watoto wawili tu.
Japo hii inaweza kuwa na kitu kizuri kwa raia wa China lakini Taasisi ya haki za binadamu Amnesty International wamesema bado haitoshi, wanahitaji Sheria iachiwe zaidi watu wawe huru kujiamulia idadi ya watoto wanaohitaji kuwa nao.
Post a Comment