Ikiwa masaa kadhaa yamesalia kabla ya klabu ya Chelsea ya Uingereza kucheza mechi na Liverpool katika uwanja wake wa nyumbani wa Stamford Bridge, huu utakuwa mchezo wa kumi na moja kwa Chelsea
ambayo hadi sasa katika michezo kumi iliyocheza imefungwa mechi tano,
imeshinda mechi tatu na kutoa sare mechi mbili na ipo nafasi ya 15
katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza.
Kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho ambaye timu yake itacheza na Liverpool
huku ikiwa na presha ya kutaka kuokoa kibarua cha kocha huyo ambaye
anatajwa kama atapata matokeo mabovu katika mchezo huo, huenda
akafukuzwa kazi, hata hivyo Mourinho
ambaye ana maneno mengi ameshindwa kuthibitisha kuwa kama anaamini timu
yake itamaliza katika nafasi nne za juu na kupata tiketi ya kucheza
michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu ujao.
“Ni
jinsi gani napambana na hii hali? ni kwa kufanya kazi sina mashaka
tutatoka katika hiki kipindi kigumu mapema lakini siwezi kuahidi kuwa
tutapata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao, na kuhusu
ulazima wa kushinda hii mechi, kwa kazi yangu huwa sishindi kila mechi
ila huwa ni lazima kushinda kwa kila mchezo”>>> Jose Mourinho
Post a Comment