Tumezoea kuona majeneza yakitumika
kuhifadhia miili ya Marehemu au watu waliofariki, uliwahi kufikiria kuna
mtu anaweza kutumia jeneza kwa biashara zake nyingine ?!!
Stori kwenye vichwa vya habari
Kenya, jamaa watano wamenaswa wakiwa kwenye mchakato wa kusafirisha
pombe haramu iliyopakiwa ndani ya jeneza, safari yote njiani wameenda
wakiwa wanaomboleza kama watu wanaosafirisha msiba !!
Kenya kumekuwa na stori nyingi sana
mfululizo zinazohusu watu kufariki, wengine kuumwa na wengine waliwahi
kuripotiwa kupata tatizo la upofu kwa sababu ya unywaji wa pombe za
kienyeji.. hiyo ilifanya Serikali ipige MARUFUKU utengenezwaji wa pombe
hiyo.
Stori kamili hii hapa kutoka Kituo cha KTN Television cha Kenya mtu wangu, ni video ya dakika 2:39 tu.
Post a Comment