Ads (728x90)

Tabs

Page

Ni stori kuhusu bongofleva na headlines zake nje ya mipaka ya Tanzania ambapo time hii ni ya Chege akiwa yuko Afrika Kusini katika maandalizi ya video ya single mpya iitwayo Sweety Sweety aliyowashirikisha Runtown na jamaa mmoja toka kundi la Uhuru.
Akiongea na ripota wa millardayo.com, Julio Batalia ambaye yuko na Chege amethibitisha kwamba wako South Africa kwa ajili ya kazi mpya >>>> ‘Tupo South Afrika katika harakati za kushoot video ya wimbo mpya wa Chege Chigunda ambayo amemshirikisha Runtown na jamaa mwingine kutoka kundi la Uhuru, mimi nipo hapa nikishiriki kama manager wa hii video kuhakikisha video inakuwa kubwa‘- Julio.
.
.
Video itafanywa na director Justin Campos wa kampuni ya Gorilla Films na leo ndio tunaelekea location kuanza kushoot, tunaomba ushirikiano mkubwa kwa sababu hii ni video iliyogharamiwa sana, tuombeane kheri ili tufanye kitu kizuri kitachopendeza na kupresent Tanzania… tuendelee kupeana support ili tufanye mambo makubwa‘ – Julio.
.
.
.
.Julio Batalia akiwa na director Justin Campos kutoka kampuni ya Gorilla Films.

Post a Comment