Peter na Paul Okoye kwa pamoja tunawajua kama P Square, ukubwa wa jina lao sio ndani ya Africa pekeyake… wana hits kibao ambazo zimewaweka kwenye ramaniya dunia pia.
Mafanikio yao yalianzia pale ambapo waliweka nguvu yao nyingi kwa kufanya muziki wakitumia lebo yao ya Square Records… December 2011 milango mingine mikubwa ikafunguka kwenye muziki wao, waliingia Mkataba kufanya kazi na lebo ya Akon Konvict Muzik.. kazi kama Beautiful Onyinye waliyomshirikisha Rick Ross na Chop My Money zilipenya sana nje ya Afrika, watu wakazidi kuwajua !!
Safari yao haikuwa rahisi, lakini unajua
siri ya wao kuifungua milango yote ya mafanikio? Kuna kitu chochote
wanachokihofia kwa sasa?
>>> “Siri
ya mafanikio yetu ni kazi. Tunafanya sana kazi.. Juhudi zote
tunazowekeza katika kazi yote ni hofu ya umaskini, tumeshaonja maisha ya
umaskini mkubwa na tunaogopa sana umaskini, ndio maana utasikia
tumewekeza hapa na kule yote ni kujikinga na umaskini.
Tumeshuhudia
wasanii waliopata umaarufu na utajiri kabla yetu lakini leo hawana
chochote cha kuonesha kwa juhudi zao, kitu hiki kinatuogopesha
sana… Tuliwahi kuishi maisha ya kubanana baba, mama na watoto nane
kwenye nyumba ya kupanga yenye vyumba viwili, chakula, ada, mavazi
vilikuwa ni tatizo sana kwetu na kipindi hicho baba yetu alitusihi sana
tuje kuwa viongozi wa maisha yetu wenyewe tusiopenda kufanya kazi chini
ya mtu na ndio maana unawaona P Square wanafanya biashara zao wenyewe
leo”.>>> Nukuu ya walichokisema P Square kwenye moja ya Interview.
Post a Comment